Ziyech apewa 'Thank You' Wydad atimkia Brazil.
Joyce Shedrack
September 7, 2026
Share :
Klabu ya Botafogo ya nchini Brazil imefikia makubaliano rasmi ya kumsajili mshambuliaji wa Morocco Hakim Ziyech kama mchezaji huru baada ya nyota huyo kuachana na klabu ya Wydad Casablanca.
Ziyech mwenye umri wa miaka 33 ambaye amefunga magoli 9 kwenye mechi 16 amejiunga na Botafogo kwa mkataba wa miaka miwili huku klabu yake ya Wydad ikitoa taarifa rasmi ya kuachana naye na kumtakia kila la kheri.





