Zouma atambulishwa timu ya Dubai
Sisti Herman
March 1, 2026
Share :

Aliyekuwa nyota wa Chelsea na West Ham United, Kurt Zouma, amekamilisha rasmi uhamisho wake kuelekea Falme za Kiarabu kujiunga na klabu ya Al Wasl.
Beki huyo raia wa Ufaransa amesaini mkataba utakaomweka jijini Dubai hadi mwaka 2026.
Usajili huu mkubwa umekuja baada ya kuhitimisha kipindi chake kifupi na klabu ya CFR Cluj ya nchini Romania, huku Zouma akitarajiwa kuleta uzoefu wake mpana wa Ligi Kuu ya Uingereza kuimarisha safu ya ulinzi ya Al Wasl.





