Zuchu amfukia Jux na Diamond akamata usukani YouTube.
Joyce Shedrack
November 25, 2024
Share :
Video ya ngoma ya Antenna iliyoimbwa na malkia wa WCB Zuhura Otham maarufu Zuchu iliyotoka Novemba 23 mwaka huu imeshika nafasi ya kwanza kwenye mtandao wa YouTube ndani ya siku moja na kuiondoa Video ya Ololofume Mi ya Juma Jux aliyomshirikisha Diamond Platnumz.
Ololofume mi ilikamata uongozi wa video namba moja YouTube kwa takribani wiki mbili sasa imeshushwa rasmi na Antenna ya Zuchu na sasa inakamata namba mbili ikiwa na zaidi ya watazamaji milioni 4.
Audio ya Antenna iliachiwa Oktoba 20, 2024 huku video yake ikitoka siku moja iliyopita kwa sasa tayari imefikisha watazamaji zaidi ya laki 5 kwenye mtandao huo wa YouTube.
Video hiyo ambayo imesifika kutokana na ubunifu mkubwa inaonyesha Zuchu akiwa mgonjwa ambapo analazimika kuingia sehemu ya kufanyia muziki unaohusishwa na tiba yake anapojaribu kutoroka anakutana na kundi la wanaume waliovaa vinyago anabadilika na kuonekana kwa sura mpya ya kuogopesha.
Unadhani video ya Antenna itakimbiza YouTube kwa muda gani ?