Zuchu kwenye jukwaa moja na Kendrick Lamar!
Eric Buyanza
December 5, 2023
Share :
Msanii wa kike wa kizazi kipya anayekimbiza kwasasa, Zuhura Omary Kopa "Zuchu" kesho jumatano atapanda kwenye jukwaa la Move Africa ambalo linaandaliwa na Global Citizen Africa kwenye ukumbi maarufu wa BK Arena jijini Kigali, Rwanda.
Onyesho hilo ambalo linamshirikisha Zuchu kama msanii pekee atakayebeba Bendera ya Tanzania, pia litamshuhudia msanii na mtayarishaji maarufu wa muziki kutoka nchini Marekani, Kendrick Lamar.