Zuchu na Diamond akanusha taarifa za ndoa yao kuvunjika.
Joyce Shedrack
June 4, 2025
Share :
Malkia wa muziki Bongo Fleva nchini kutoka lebo ya WCB Wasafi Zuchu amefanya mabadiliko katika utambulisho wake wa Instagram ‘Bio’ na kutaka afahamike rasmi kwa jina la Mrs Nasibu.
Hii ni mara baada ya kukaa kimya kwa siku kadhaa tangu Diamond atangaze kuwa alishawahi kumuona Zuchu miezi michache iliyopita kwa ndoa ambayo ilikuwa na siri kubwa.
Kwa upande wa staa wa muziki Diamond Platnumz ameendelea kusisitiza kuwa yeye ni mume wa mtu ambapo usiku wa kuamkia leo wakati alipokuwa akitumbuiza kwenye Mkesha wa Mwenge uliyofanyika Ilala alithibitisha hilo.
“Niwaambie kitu siku ya leo mimi sikuwa vizuri kwenye afya nilikuwa najisikia kuumwa umwa, unajua ukishakuwa ndani ya ndoa kuna kanamna yani si niwaache mambo ya Mwenge yaendelee. Mimi ni mume wa mtu jamani nyie nina kazi maalumu muda huu, hamuwezi kunielewa kwa sababu hamjaoa na kuolewa sasa ukioa ndio utanielewa,”amesema Diamond.
Haya yaliyojiri kwa hivi sasa kwa wanamuziki hao wawili yanazima uvumi uliokuwepo kwamba licha ya wawili hao kufunga ndoa miezi kadhaa nyuma lakini tayari wamepeana talaka.