Zulia jekundu la rais wa Malawi lililoibiwa lapatikana
Eric Buyanza
January 26, 2024
Share :
Polisi nchini Malawi wamepata zulia la Rais lililokuwa limeibiwa siku ya Jumatano.
Zulia hilo liliibwa pamoja na hema usiku wa kuamkia Jumatano wakati bidhaa hizo zikihamishwa kuelekea sehemu ambayo Rais Chakwera alitarajiwa kufanya hafla.
Watu wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo, na wanashukiwa hao inalezwa kwamba waliiba vitu hivyo kutoka kwenye gari la Wizara ya Uchukuzi lilipokuwa likisafirisha vifaa hivyo.