pmbet

Zuma azuiliwa kugombea Urais Afrika Kusini

Eric Buyanza

March 29, 2024
Share :

Tume ya uchaguzi nchini Afrika ya Kusini imemuondoa rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma kwenye kiny’anganyiro cha kugombea urais kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu, na hivyo kuzua mvutano katika maandalizi ya uchaguzi huo.
 

Hata hivyo katika hali ya kushangaza tume hiyo haijatoa sababu za kumuondoa.
 

Nchi hiyo itafanya uchaguzi mkuu tarehe 29 Mei, uchaguzi ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994.

Chama tawala cha African National Congress(ANC) kiko kwenye hatari ya kupata chini ya asilimia 50 ya kura kwa mara ya kwanza tangu kilipoingia madarakani mwishoni mwa enzi ya utawala wa makaburu.
 

Zuma, mwenye umri wa miaka 81, alilazimika kuondoka madarakani mwaka wa 2018 kwa tuhuma za ufisadi lakini bado ana umaarufu mkubwa wa kisiasa nchini humo.
 

Amekuwa akifanya kampeni na chama cha upinzani cha uMkonto we Sizwe (MK) katika jaribio la kurudisha tena hadhi yake, akiwaita wanachama wa chama chake cha zamani cha ANC, “wasaliti”.
 

Uungwaji mkono wake kwa chama kipya cha Umkhonto we Sizwe (MK) umeonekana kuwa tishio kwa chama tawala cha African National Congress (ANC).

Bwana Zuma anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa tume ya uchaguzi kabla ya tarehe 2 Aprili.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet